Ulaji mzuri wa samaki unategemeana na hali ya hewa hususani katika hali ya joto la wastani na vipindi vya jua.
Mara tu yatokeapo mabadiliko ya hali ya hewa uathiri sana mfumo mzima wa ulaji wa samaki katika kula. Pia hali ya baridi sana na ikiwemo mabadiliko ya ghafla katikahali ya hewa hupelekea ulaji wao kuwa mdogo na wakati mwingine kutokula kabisa.
Kwa kawida samaki hawali vizuri katika hali ya misukosuko (stress) ambayo husababishwa na viumbe wala nyama (predators) ambao watakuwa bwawani, uvunaji wa mara kwa mara katika bwawa (kuingia ndani ya maji), kutokuwa na maji bora na salama n.k. Pia ongezeko la joto ambalo ni tatizo na pia upelekea upungufu wa hewa ya oxygen katika maji.
NAMNA YA ULISHAJI SAMAKI
Kawaida jamii ya samaki aina ya sato/perege hula kwa kutupia chakula ndani ya bwawa lako. Ni vyema kukawa na maeneo maalumu ya kulishia au kutengenezea maeneo mbadala ya kuwekea chakula cha samaki bwawani hii itasaidia kuweza kujua iwapo samaki wako wanakula au la, pia itawapa uzoefu wa wao kujua sehemu chakula kinapopatikana wakiwa bwawani.
Umuhimu wa kutenga maeneo mbadala ya kulishia ni hupelekea mara tu uwekapo chakula samaki hutambuana mara moja na kuanza kula chakula hicho. Chakula hicho Pia katika bwawa dogo kuwe na sehemu moja ya kulishia isipokuwa katika mabwawa makubwa kuwe na sehemu nyingi za kulishia ambazo hazibadilishwi.
Wataalamu tunashauri kuwa ni vyema kutowapa chakula wakati wa mvua, wakati wa usiku na wakati wa wingu zito hii itasaidia kuto kupoteza chakula bure na kupunguza gharama kwa sababu wakati huu samaki ulaji wao ni mdogo sana na pengine hawali kabisa.
By Clemence Francis
No comments:
Post a Comment