Upatikanaji wa vifaranga wa samaki na namna ya usafirishaji hadi sehemu ya kufugia (bwawani). Samaki wanaweza kusafirishwa wakiwa hai kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na mahitaji husika. Usafirishaji wa samaki hai unaweza kuhusisha samaki wa kubwa au samaki wadogo (vifaranga wa samaki). Kuna njia tofauti tofauti za usafirishaji wa vifaranga wa samaki kulingana na umbali na kiwango cha uchumi cha mfugaji au muuzaji wa vifaranga wa samaki. Katika kusafirisha samaki kuna mambo muhimu ya kuzingatia kama ifuatavyo:-
1. Umbali na muda wa kusafirisha. Umbali wa kutoka eneo wanapochukuliwa samaki hadi eneo la ufugaji unapokua kua mfupi hupunguza muda wa kusafilisha vifaranga wa samaki na kujihakikishia kiwango kikubwa cha samaki kuendelea kuishi kwa sababu ubora wa maji yanayosafirishiwa huwa umepungua kwa kiasi kidogo, lakin umbali unapokua mkubwa hupunguza uwezo wa samaki kuishi kutokana na kupotea kwa ubora wa maji yanayotumika kusafirishia kutokana na taka mwili zinazotolewa na samaki.
2. Kiwango cha joto la maji: joto la maji linapaswa kuwa la kuvumilika na samaki (joto la wastani) kwa sababu kiwango cha joto la maji kinapo ongezeka hupunguza hewa ya oksijen kwenye maji na kupelekea vifo kwa samaki. Kiwango kizuri cha joto la maji ya kusafirishia samaki kiwe ni nyuzi joto 18-32 C.
3. Njia ya usafirishaji: njia ambayo ni ya haraka na rahisi kulingana na sehemu husika hutoa nafasi ya kufanikisha zoezi la usafirishaji. Njia za usafirishaji na vyombo vya kusafirishia. Vyombo vinavyotumika katika usafirishaji wa samaki hutofautiana kwa ukubwa, aina na idadi ya samaki wanaotakiwa kusafirishwa.
kuna aina mbili za usafirishaji samaki, nazo ni kama ifuatavyo
a) Njia ya vyombo vya wazi: njia hii hujumuisha vyombo vyote ambavyo havizibwi juu ili kuruhu hewa kuingia, njia hii hupunguza kubadilisha maji wakati wa safari, pia njia hii ni nzuri kwa usafirishaji wa umbali mfupi.
b) Njia ya vyombo vilivyofunikwa: njia hii hujumuisha vyombo vyote ambavyo hufunikwaa au kufungwa. Njia hii pia inaweza tumia mifuko ya nailoni ambayo hufungwa ikiwa na sehemu ya hewa ndani yake au matanki ambayo hujazwa maji nusu kulingana na idadi ya samaki na kuacha nafasi ya hewa. Njia hii ni nzuri kwa usafirishaji wa samaki wengi na kwa umbali mrefu.
4. Kuwaandaa samaki kabla ya usafirishaji kwa kutowalisha siku mbili kabla ya safari ili kuepusha uchafuzi wa maji ya kusafirishia kwa taka mwili na pia kupunguza shughuli za kimwili za samaki.
5. Kuweka hewa ya oksijeni ya kutosha kulingana na idadi ya samaki
6. Kuhakikisha vyombo vilihifadhi samaki haviyumbi yumbi wala kuhama hama wakati wa usafirishaji.
7. Badilisha maji mara kwa mara endapo utaona hamna hewa ya oksijeni ya kutosha.
8. Joto la maji lisiwe kali ili kuwezesha kuwango kikubwa cha hewa ya oksijeni kuchanganyika na maji( nyuzi joto 18-32)
9. Kuwazoesha samaki mazingira mapya ili kuweza kuepusha vifo vya samaki kutokana na ugeni/mabadiliko ya mazingira.
Sababu zinazoweza kusababisha vifo vya samaki wakati wa usafirishaji
- kuongezeka kwa joto la maji zaidi ya kiwango hitajika
- Kupungua kwa hewa ya oksijeni kwenye maji
- kupungua kwa ubora wa maji kutokana na wingi wa taka mwili za samaki.
Endapo utakutana na changamoto ya kupanda kwa joto la maji tumia barafu kuweza kushusha joto la maji hadi kwenye kiwango hitajika, pia barafu zisiwekwe moja kwa moja kwenye chombo cha kusafirishia samaki bali ziwekwe pembezoni mwa chombo hicho hii husaidia kupunguza hali ya joto kwa taratibu kuepusha kushuka kwa joto ghafla.
No comments:
Post a Comment