Thursday, June 23, 2022

NAMNA BORA YA USAFIRISHAJI WA SAMAKI

 Upatikanaji wa vifaranga wa samaki na namna ya usafirishaji hadi sehemu ya kufugia (bwawani). Samaki wanaweza kusafirishwa wakiwa hai kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na mahitaji husika. Usafirishaji wa samaki hai unaweza kuhusisha samaki wa kubwa au samaki wadogo (vifaranga wa samaki). Kuna njia tofauti tofauti za usafirishaji wa vifaranga wa samaki kulingana na umbali na kiwango cha uchumi cha mfugaji au muuzaji wa vifaranga wa samaki. Katika kusafirisha samaki kuna mambo muhimu ya kuzingatia kama ifuatavyo:-

Thursday, May 26, 2022

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUCHAGUA ENEO LA KUCHIMBA BWAWA LA SAMAKI

 Bwawa la samaki linalo chimbwa ardhini (earthen pond) huitaji uangalifu wa hali ya juu katika utengenezaji ili kuweza kuepusha hasara ambazo zinaweza kumpata mfugaji. Ukubwa wa bwawa unategemea na ukubwa wa eneno la mfugaji na uwezo wa kifedha alionao mfugaji wa samaki, ingawa inashauriwa kuanz na bwawa lenye ukubwa wa mita mraba 200 kama unafuga samaki wa biashara na kama unafuga samaki wa chakula nyumbani unaweza kuanza na bwawa la ukubwa wowote kulingana na mahitaji yako. Ili uweze kuchagua eneo zuri kwaajili ya bwawa la samaki ni lazima kuzingatia vigezo vifuatavyo.

Upatikanaji wa maji ya uhakika na yaliyo safi na salama Bila kujali mfumo au aina ya samaki anae fugwa maji ya kutosha, yenye ubora na yanayoweza kupatikana kwa mwaka mzima ni muhimu katika ufugaji wa samaki ambapo maji yanaweza kuwa ni ya kisima, mto, ziwa, maji ya bomba, chemchem au maji ya mvua (maji yasiwe ya chumvi) kwa samaki wa maji baridi mfano sato, kambale n.k.

Mandhali ya nchi (topography) Muonekano wa eneo ni muhimu sana katika uchimabaji wa bwawa, eneo lenye muinuko au mteremko mkali halishauriwi katika ujenzi wa bwawa pia eneo lenye bonde huwa na hatari ya kupatwa na mafuriko ikitokea kukawa na mvua kubwa.

Eneo la bwawa la samaki linapaswa kuwa mbali na shughuli za viwanda ili kuepusha kemikali zinazotokana na viwanda kuweza kuwadhuru samaki hivyo kupelekea kupunguza ubora na ukuaji wa samaki na mda mwingine hata kupelekea vifo vya samaki.

Bwawa la samaki liwe sehemu inayoweza kufikika kwa urahisi wakati wote katika majira ya mwaka ili kuweza kurahisisha usafilishaji wa samaki kwenda sokoni.

Eneo lisiwe na mogogoro yoyote na jamii ili kujihakikishia usala wa samaki katika kipindi chote cha uzalishaji.

Sehemu yenye udongo bora na unaohifadhi maji kwa muda mrefu (udongo mfinyanzi) ambapo husaidia kupunguza upotevu wa maji pia kupunguza garama za uingizaji maji katika bwawa, katika kuchagua aina ya udongo kuna majaribio tofauti tofauti uanayoweza kuyafanya ili kujua ubora wa udongo kama ifuatavyo:

Njia ya kwanza.

Chukua udongo lowesha maji kidogo yanayoweza ruhusu udongo kushikana kasha tengeneza tonge la udongo kwa kufinyanga kwanguvu kisha lirushe juu na uliache lianguke ardhini, kama donge la udongo halitasambaa basi udongo huo utakua ni mzuri na una uweo wa kutunza maji.

Njia ya pili

Chimba shimo linalofika usawa wa mita moja kisha chukua udongo wa ndani ya shimo na ujaribu kama unafaa kwa kufuata njia namba moja kwa kurudia rudia mara kadhaa ili kuweza kujiridhisha kama udongo unafaa.

Njia ya tatu

Chimba shimo lenye uref wa mita moja au zaidi na ujaze maji kujaa shimo na ulifunike kisha uyaache hayo maji kwa masaa 24 baada ya hapo njoo uangalie kiwango cha maji kilichopungu, rudia tena zoezi la kujaza maji katika shimo na uliache kwa saa 24 kisha urudi tena kuangalia kiwango cha maji kilichopungua, na kama kiwango cha maji yaliobaki yatakua ni mengi kuzid yaliopungua basi eneo hulo lina faa kwa kuchimba bwawa.

NAMNA BORA YA KULISHA SAMAKI

Lisha chakula bora cha samaki husika, wengi tunakosea, chakula cha sato tunawalisha kambale, chakula cha samaki wadogo tunalisha samaki wakubwa au chakula cha samaki wakubwa tunalisha samaki wadogo, hii inapunguza na kuondoa ufanisi katika ufugaji wa samaki Je, chakula unacholisha ni sahihi kwa samaki ulionao..??? 

UKUAJI WA SAMAKI

Lengo la mfugaji wa samaki ni vifaranga alivyovipandikiza bwawani vikue haraka ili viweze kufikia uzito unaotakiwa mapema inavyowezekana na, kwa hiyo, kuvunwa mapema kusudi kuokoa gharama za kuwatunza na kuwalisha kwa kipindi kirefu.

Ukuaji wa samaki bwawani huathiriwa na mambo kadhaa, makubwa yakiwa ni haya yafuatayo: